ads

Rais Magufuli amewazungumzia wabunge wawili wa (CHADEMA) Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na Mbunge  wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari kuwa ni wabunge halali wa majimbo hayo kwa kuwa wananchi ndiyo waliwachagua.


Rais Magufuli amesema hayo  aliposimamishwa na wananchi wa Sangisi katika kata ya Akeri nje kidogo ya Mji wa Arusha akiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam leo Asubuhi na kusema yeye atabaki kuwa Rais wala hawezi kubadilika na kuendelea kuwatumikia Watanzania wote. 

"Uchaguzi umeshakwisha sasa ni maendeleo mliamua mkamchagua Magufuli na ndiyo Rais na mimi nitakuwa Rais wala sibadiliki na nitawatumikia Watanzania wote, mliamua mkamchagua Mhe. Lema wa CHADEMA kuwa Mbunge wenu yule ni Mbunge halali, mkaamua kumchagua Nassari kuwa Mbunge wenu ni Mbunge halali kwa hiyo tushikamane sisi kama Watanzania kuleta maendeleo yetu uchaguzi ulikwisha tusubiri mwaka 2020" alisema Rais Magufuli 

Mbali na hilo Magufuli amewataka Watanzania kuleta maendeleo ya kweli bila kubagua vyama na kubagua dini zetu na bila kubagua makabila na kusema yeye kama kiongozi wa nchi hajaweza kuwabagua na ndiyo maana anafanya mambo ya maendeleo katika majimbo hayo ikiwa ni pamoja na kupeleka barabara 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: