Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye hatambuliwi na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Maalim Seif Sharif Hamad amezungumzia tena ndoto yake ya kukabidhiwa nchi hivi karibuni.
Akizungumza katika kongamano la vijana wa vyuo vikuu wa CUF juzi, Maalim Seif aliwataka wafuasi wa chama hicho kutokata tamaa sasa kwani haki yao "iliyoporwa Oktoba 25, 2015 itapatikana" na yeye atakabidhiwa madaraka ya Rais wa Zanzibar.
“Niwatoe wasiwasi," alisema Maalim Seif katika hotuba yake. "Ingawa wenzetu (CCM) wanakwenda mbio, angalau waoengezewe siku ili wasiondoke madarakani."
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaongozwa na Rais Dk. Ali Mohammed Shein wa Chama cha Mapinduzi.
Maalim Seif aliwataka wafuasi wa chama hicho kuendelea kutulia kwani haki yao ipo na atakabidhiwa urais wa Zanzibar siku chache zijazo, chini ya uangalizi wa kimataifa.



Post A Comment: