ads

Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba imemtua Dr. Arnold Kashembe kuwa katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo baada ya kamati hiyo kukaa kikao jana jioni.


Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Kaimu wa rais klabu hiyo, Salim Abdallah na kusema uteuzi wa Katibu Mkuu huyo mwenye shahada ya uzamivu na aliyekuwa Mhadhiri kwenye vyuo mbalimbali barani ulaya  unaanza kufanya kazi mara moja.

Pamoja na hayo, Salim amewataka wanachama na mashabiki wa wekundu wa Msimbazi kuendelea kuwa na utulivu,hususani kipindi hiki ambacho baadhi ya viongozi wao wakiwa kwenye shauri lao,liliopo Mahakamani dhidi ya mashtaka yanayowakabili.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: