ads

Nyota wa soka wa England Wayne Rooney, ambaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United na kurejea Everton amesema anasubiri kwa hamu sana kuzuru Tanzania.


"Naisubiri sana kwa hamu na ghamu (safari ya kwenda Tanzania) - inafaa kuwa safari nzuri," aliambia runinga ya evertontv.

"Itakuwa nzuri sana na natumai kwamba nitaweza kuingia uwanjani na kucheza.

"Huwa vizuri sana unaposafiri na timu. Ni vizuri kuwa hotelini na wachezaji, kujumuika nao na kuwafahamu zaidi.

"Sijawahi kwenda Tanzania, na kwa hivyo nasubiri sana kwenda huko."

Rooney atakuwa kwenye kikosi cha Everton kitakachocheza mechi ya kujiandaa kwa msimu ujao katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Amesema ziara hiyo itampa fursa mwafaka ya kufahamiana na wachezaji wenzake wapya.

Rooney, anayeongoza kwa ufungaji mabao England alitia saini mkataba wa miaka miwili Goodison Park Jumapili.

Rooney alifika kwa mazoezi USM Finch Farm leo Jumatatu na anapangiwa kuungana na wenzake kwa safari hiyo ya Tanzania baadaye wiki hii.

Credit - BBC

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: