ads

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) , Dionis Malinzi, ambaye ni ndugu na Rais wa Shirikisho la Soka Jamali Malinzi ametumbuliwa leo na Waziri wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Mwakyembe kufuatia agizo la Waziri Mkuu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimtaka Waziri Mwakyembe kupitia baraza hilo na kulitathimini hivyo baada ya kulipitia na kutathimini amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa baraza hilo. 

"Kwa mamlaka niliyopewa na sheria ya BMT Na. 12 ya 1967, nimesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wote wa BMT"- Dkt.Harrison Mwakyembe

Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe amesema kuwa Sekretarieti ya Baraza la Michezo Tanzania litaendelea na kazi kwa kushirikiana na serikali wakati mchakato wa kuteua mwenyekiti mpya wa baraza hilo ukiendelea.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: