ads

MGANGA wa jadi, Levocatus Kanjalanga (65), ameuawa kwa kuchomwa na mkuki mgongoni na mtu ambaye anadaiwa kuwa ni mteja wake wa muda mrefu.


Ilielezwa na mashuhuda kuwa mtu huyo alikuwa akimlalamikia mganga huyo kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akimtibu kwa kumtoza fedha nyingi, lakini haponi maradhi yanayomsumbua.

Mtoto wa mganga huyo aliliambia gazeti hili kuwa baba yake aliuawa juzi saa 1:30 asubuhi kwa kupigwa mkuki  mgongoni akiwa anatembea mitaani katika Kitongoji cha Chawe kilichopo katika Mji wa Namanyere  wilayani humo. 

Alisema kwa muda mrefu watu ambao walikuwa wakitibiwa na baba yake walikuwa wakilalamika kutozwa fedha nyingi pamoja na mifugo, lakini hawaponi, hali iliyosababisha kuanza kumuona kama tapeli.

Alisema watu hao walikuwa wanalalamikia na kutofanikiwa matatizo yao ya kiafya, kutafuta mali pamoja na mazindiko.

“Pengine malalamiko hayo ndiyo yaliyosababisha mtuhumiwa aamue kumuua kwa kumchoma mkuki mgongoni, na aliyefanya tukio hilo hajapatikana na mkapa sasa anatafutwa,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anasakwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: