ads

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imekutana leo Jumamosi Julai 01, 2017 kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam imempitisha Wallace Karia kuwa Kaimu Rais wa shirikisho hilo huku Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi kuwa Kaimu.


Viongozi hao watakaimu nafasi tajwa hapo juu hadi mahakama itakapotoa maamuzi kuhusu kesi zinazowakabili kwa sasa ambaye ni  Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine. 

Kamati ya Utendaji ya TFF, imekutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6) na kufanya uamuzi huo.

Katika hatua nyingine, Karia amesema ujumbe wa FIFA unakuja nchini kufuatilia sakata zima la viongozi hao wa TFF kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: