Rais John Magufuli amesema utafikia wakati ambapo wabunge watakataa kuteuliwa kuwa mawaziri kwa kuogopa kasi ya utendaji wake.
Akizungumza jana Jumapili Julai 23, Rais Magufuli amesema mawaziri anaowateua ni lazima wakubali matendo anayoyataka kwa sababu ndiyo wananchi wanayoyataka.
“Tumechezewa vya kutosha, waziri lazima afanye yale ninayotaka mimi, ingawa hata hawa niliowachagua hakuna aliyekataa,” amesema.
Amesema Tanzania imechezewa kwa muda mrefu na kusababisha watu kukosa mapato yanayotokana na rasilimali za nchi.
“Tumechezewa vya kutosha, mimi ndiyo rais wa nchi hii na ninawaambia kweli kuwa tumechezewa, rais anajua siri za nchi,” amesema.
Post A Comment: