Solomon L laizer diwani Kata ya Ngabobo Wilayani Arumeru kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) amejiuzulu hivi punde.
Katika barua yake kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Laizer anakiri kuridhishwa na kazi kubwa anayoifanya Mhe Rais Magufuli ambayo imeiletea heshima kubwa nchi yetu, na kudai kuwa kuendelea kukaa CHADEMA ni kuisaliti nafsi yake.
Awali katika mahojiano, Laizer anampongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg Alexander Mnyeti kwa kazi ya heshima anayoifanya na kumuomba amfikishie salamu kwa Rais Magufuli kwamba wananchi wa Ngabobo wanamuelewa sasa kuliko wakati wowote.



Post A Comment: