ads

MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Kassim Dewji, amekataa kuteuliwa kukaimu nafasi ya urais wa klabu hiyo kama katiba ya klabu hiyo inavyosema, imefahamika.


Dewji, Katibu Mkuu wa zamani wa klabu hiyo ni mjumbe wa kuteuliwa na ndiye mkongwe kulinganisha na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji ya Simba waliobakia.

Taarifa zilizopatikana kutoka katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana asubuhi, zinaeleza kuwa Dewji amekataa kukaimu nafasi hiyo ya Evans Aveva kutokana na kutotaka kuwagawa wanachama wa klabu hiyo.

"KD ( Kassim Dewji) amekataa kukaimu nafasi ya Evans kwa lengo la kutaka wanachama wasigawanyike, pia ana sababu zake binafsi ambazo zinamzuia kukubali kulibeba jukumu hilo," kilisema chanzo chetu.

Mbali na nafasi ya Aveva, pia wajumbe wanatakiwa kutangaza mjumbe atakayerithi nafasi ya Makamu wa Rais, Geofrey Nyange "Kaburu" ambaye kwa pamoja na Aveva wapo mahabusu wakikabiliwa na mashtaka matano ya utakatishaji fedha za klabu.

Mbali na Dewji, wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji ya Simba waliopo ni Mohammed Nassor, Salim Abdallah, Meddy Milanzi, Mulamu Nghambi, Jasmine Soudy, Said Tully, Ally Suru na Iddi Kajuna.

Aveva na Kaburu wapo rumande hadi Julai 13, mwaka huu kesi yao itakaposikilizwa tena, jambo ambalo linaifanya Simba kuwa katika wakati mgumu kutokana na viongozi wao hao wa juu kukosekana.

Hatua ya Kamati ya Utendaji ya Simba kukutana na kupendekeza baadhi ya wajumbe kukaimu nafasi hizo ni kutokana hasa na suala zima la usajili katika kipindi hiki na maandalizi mazima ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: