TAKUKURU imesema inawashikilia Harbinder Singh Sethi na Jemes Rugemalila kwa makosa ya uhujumu uchumi. Wanapelekwa kwenye mahakama ya kisutu na baadae watapelekwa Mahakama ya Maalumu ya kifisadi


"Ndugu wanahabri, leo tumekutana tena mchana huu, ili kuwapeni taarifa za Mapambano yetu dhidi ya rushwa na Ufisadi nchini. Na leo tunawapa taarifa kwamba tunawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili, Bwana Harbinder Singh Sethi na bwana Jemes Rugemalila. Hawa tunawafikisha mahakamani kwa Kosa la uhujumu Uchumi na makosa mengine yanayofanana na hayo. Kwa muda mrefu sana nmekuwa naulizwa, Kesi za Escrow zimeishia wapi, Kesi ya IPTL imeishia wapi. Kama tulivyowahi kusema Mwanzo kwamba Taasisi ya kuzuia na kupambana na ruswa, inajukumu la kimsingi la kupambana na rushwa na makosa ya ufisadi. Kwahiyo katika muendelezo wa majuku yetu,tulichunguza shauri hili kwa muda mrefu, Sasa imefika muda muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa wakuu hawa wa mashauri hayo ya uhujumu uchumi wa nchi yetu mahakamani.

Kwa hiyo tayari wameshapelekwa mahakamani, na nitoe wito kwa wananchi kwamba Serikali ina nia ya dhati ya kupambana na vitendo vya uhumumu uchumi wa Nchi yetu ili wananchi wapate maisha bora zaidi. Na jukumu hili TAKUKURU itaendelea kulitekeleza kwa nguvu zetu zote, kwa waledi wetu wote na kwa umakini wa hali ya juu ili kuhakikisha kwamba vitendo vya hujuma dhidi ya uchumi wa nchi yetu vinadhibitiwa ili wananchi wapate Maisha Bora".
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: