ads

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, kufuatia kifo cha Mzee Ndessamburo kwa kuweka wazi kwamba ni kiongozi ambaye alikua mchapakazi kwa wananchi wake.


“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mh. Ndesamburo ambaye pia ni baba wa Mbunge wa Viti Maalumu Lucy Owenya kilichotokea mkoani Kilimanjaro hakika ni pigo kubwa” Alisema

Aidha Mh. Ndugai amesema kuwa marehemu Ndesamburo, aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Moshi mjini mwaka 2000 - 2015 atakumbukwa kwa uchapakazi wake wakati akiwa mbunge hasa katika kuwaletea wananchi wa jimbo lake maendeleo.

Mhe. Ndesamburo aliyezaliwa 19 Februari 1935, amefariki leo tar 31 Mei 1935 akiwa hospitali ya KCMC mjini Moshi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: