ads

Rais John Magufuli ameeleza sababu ya kumteua Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro huku akimhimiza akachape kazi.


Rais Magufuli ametaja sababu hiyo wakati wa hafla ya kumwapisha Mghwira iliyofanyika leo, Jumanne jijini hapa na kuhudhuriwa na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro,”amesema Rais Magufuli na kuongeza;

“Wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi.”

Rais Magufuli amemhakikishia kuwa atapata ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake na asikubali kuyumbishwa na mtu yeyote katika majukumu yake.

Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Saidi Meck Sadiki aliyekuwa mkuu wa mkoa huo.

Kwa upande, Mghwira amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na amemuahidi kuwa yupo tayari kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kujenga Taifa.

“Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu, kumekuwa na minong’ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo,” amesema Mghwira. 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: