Wingu la mauaji limezidi kutanda katika Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani. Taarifa zinasaema kiongozi mwingine wa CCM ambaye ni mjumbe wa shina, ameuawa katika kijiji cha Ikwiriri na watu wasiojulikana na mwili wake kutelekezwa eneo la Daraja tatu Wilayani humo.
Akizungumza na Mtanzania jana Ndugu wa Marehemu, Isaka Hamis alimtaja ndugu yake aliyeua kuwa ni Masunga Mayuka.
Nlipokea taarifa za tukio hilo leo(jana) asubuhi wakati huo nikiwa nyumbani kwangu. Mdogo wangu ambaye anaishi Ikwiririndiye wa kwanza kunijulisha juu ya tukio hilo, alinipigia simu, alisema Isaka.
Alisema kwa mjibu wa Maelezo ya mdogo wake huyo, ndugu yao aliuawa akiwa njiani kwenda Msikitini kufanya ibada.
" Mdogo wangu alinieleza, inadaiwa Mayuka alikutana na wauaji njiani ambao walimpiga Risasi na baada ya kitendo hicho walitokomea kusikojulikana" alisema.
Alisema saa chache baada ya kupokea simu ya mdogo wake huyo, alipokea tena simu ya ndugu yake mwingine ambaye naye alimjulisha jambo hilo hilo la kusikitisha.
"Nlielezwa kwamba ndugu yangu aliuawa huku akiwa anajitetea mbele ya watu hao Wasimdhuru, Sasa tupo msibani tunajiandaa kwa maziko" alisema Isaka.
Akizungumza na Mtanzania Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga, alise,a hajapokea taarifa hizo na kuahidi kuzifanyia kazi. "Sina hizo taarifa, sijazipokea labda na mimi nizifuatilie hivi sasa". alisema.
Tangu mauaji hayo yatokee, inadaiwa watu takriban 38 wamekwisha kuuawa.
Chanzo: Mtanzania
Post A Comment: