ads

BAADA ya mwaka jana kula shavu la ku­cheza tamthiliya nchini Kenya kwa mwaka mmoja ambalo limeisha mwezi huu, staa wa fil­amu Bongo, Yusuf Mlela amejikuta akichekelea baada ya kupata kazi ny­ingine tena.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Mlela alisema ana furaha kubwa kupata kazi nyingine inayokwenda kwa jina la Nyota ambayo ni ya miezi saba watai­fanya na wasanii wa Kenya pamoja na wa Tanzania ambao ni Daud Michael ‘Duma’, Salama Salmini ‘Sandra’ na Hasheem Kambi.

“Nimefurahi sana kwa kweli maana kazi ya kwanza ndiyo nimemaliza mwezi huu sasa nimepata nyingine ambayo tut­aifanya kwa miezi saba, najiona mwenye bahati sana kwa kweli maana Kenya ninajifunza mam­bo mengi yanayohusiana na filamu, lakini pia nitatengeneza pesa zaidi kupitia kazi yangu hii,” alisema Mlela.

Credit - Risasi
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: