ads

    Kutokana na uchovu wa kutafuta maji, wanawake mkoani Mara hushindwa kuwapa unyumba waume zao.


    Hayo yamesemwa leo Jumatatu na Mbunge wa Viti Maalum mkoani humo, Agnes Marwa alipokuwa akichangia bajeti ya Serikali bungeni.

    "Ikifika jioni, wanawake mkoani Mara hushindwa kuwapa unyumba waume zao. Naomba Serikali iangalie namna ya kumtua ndoo mwanamke," amesema Agnes.

    Uhaba wa maji ni hoja iliyoibuliwa na wabunge wengi wanaoitaka Serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya miradi yake ili kumaliza kero hiyo.

    Serikali imeshauriwa kuimarisha mfuko wa maji vijijini kwa kutafuta vyanzo vya uhakika vya mapato ili kufanikisha hilo.
    ads
    Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
    Share To:

    SWAHIBA MEDIA STAFF

    Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

    Post A Comment: