Rais John Pombe Magufuli (JPM) amekutana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni mama ya uchimbaji wa madini ya Barrick Canada, Profesa John Thornton na kufanya naye mazungumzo Ikulu leo.
Amesema Barrick imepitia mapendekezo yote ya kamati ya pili ya mchanga wa madini na kuwa imekubali kulipa chochote ambacho kitaonekana wanatakiwa kulipa.
“Baada ya kuwaona nilifurahi na nikasema hawa ni wanaume, wakasema yaliyotokea ni bahati mbaya na wanatubu kwa hayo.” Amesema
Rais amesema baadaye Barrick watakuja na timu yao ya wanasheria wakati kwa upande wa Tanzania nao itakuwepo timu ya wanasheria wakiongozwa na Profesa Palamagamba Kabudi.
“Itakuwa ni timu ya maprofesa kwa maprofesa,” amesema.
Amesema timu hiyo ya Barrick ilipitia mapendekezo yote na wakakubali kuwa wapo tayari kulipa baada ya majadiliano na makubaliano yatakayoafikiwa.
Post A Comment: