Makampuni ya Japan yanafahamika kwa kuwa na muda mrefu zaidi wa kazi pamoja na misongo ya mawazo inayowakabili wafanyakazi wake, na sasa baadhi yamedai kuwa waajiriwa wapya ambao ni wanyama ‘paka’ na ‘mbwa’ wanaweza kuwa dawa ya matatizo hayo.
Kampuni ya Workaholic inayotajwa kwa kuwa na muda mrefu zaidi wa kazi, imedai kuwa tangu iwaajiri wanyama hao ufanisi wa kazi umeongezeka.
Wanyama hao huongeza furaha na ‘kampani’ kwa wafanyakazi.
Hidenobu Fukuda, kiongozi mkuu wa kampuni hiyo amesema kuwa amekuwa akiwalipa mishahara paka na mbwa hao wanaoingia ofisini, na kwamba anaridhishwa na kazi wanayoifanaya kwani hata baadhi ya wafanyakazi wamekiri kupunguza msongo wa mawazo.
“Mbali na mishahara, pia huwa ninalipa ¥5,000 ($45) kila mwezi kwa wote wanaoangalia usalama wa paka hao,” alisema Fukuda.
Alisema kuwa watumishi hao wapya ambao kazi yao kubwa ni kuwafariji na kuwapa kampani wafanyakazi ofisini, wamefunguliwa akaunti kwenye mitandao ya kijamii.
Post A Comment: