ads

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amefanya ziara katika maeneo ya Kibiti na Mkuranga kutimiza ahadi baada ya kuombwa na wazee wa maeneo hayo kufuatia mauaji ambayo yamekuwa yakiripotiwa kutokea mara kwa mara.


Mara baada ya kuzungumza na wazee hao, IGP Sirro amesema kuwa wazee hao wametoa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na namna ya kuwapata waharifu ambao wamekuwa wakifanya mauaji katika maeneo hayo.

Sirro amewaahidi wananchi wa maeneo hayo kuwa atatoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa raia mwema atakayetoa taarifa sahihi kwa watu wanaofanya mauaji mkoani. Tazama hapa
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: