ads

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amekula kiapo Ikulu jijini hapa jana, Jumanne Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kitajadili utekelezaji wa majukumu yake mapya na ya uenyekiti wa chama hicho.


ACT imesema ilipokea taarifa ya uteuzi huo wakati Mghwira akiwa nje ya nchi hivyo baada ya kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho pamoja na yeye walifanya mazungumzo kuhusu uteuzi huo.

Mghwira aliteuliwa nafasi hiyo Juni 3, mwaka huu na Rais John Magufuli kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Saidi Meck Sadick aliyeamua kuachia ngazi ili vijana waendelee kufanya kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Jumanne na kuthibitishwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT, Ado Shaibu ni kuwa kufuatia uteuzi huo na uenyekiti na majukumu ya Mkuu wa Mkoa kamati ya uongozi wa chama itakutana leo kwa ajili ya mazungumzo.

Pamoja na mambo mengine chama kitajadili namna ambavyo Mghwira atatekeleza wajibu wake wa uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya.

 “Chama kinatoa wito kwa wanachama wake kuendelea na utulivu wakati wa vikao vyake vya chama vinachukua hatua stahiki kuhusu jambo hilo,”imesema taarifa hiyo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: