Rais John Pombe Joseph Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton Ikulu jijini Dar es salaam. Katika mkutano huo, uliohudhuriwa pia na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles umemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo pande zote zimekubaliana kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya madini. Habari kamili yaja punde
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Post A Comment: