Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imesema imetambua mazungumzo yaliyofanyika kati ya Rais John Magufuli na Mkurugenzi Mtendaji wa Barrick Gold, John Thornton.
Acacia wamesema wanatambua uwepo wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Tanzania mapema leo kufuatia mkutano kati ya Rais wa Tanzania, Mh. Dk John P. Magufuli na John Thornton, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation.
Acacia wametoa taarifa hiyo leo, saa chache baada ya Rais kufanya mazungumzo na Mkurugenzi huyo wa Barrick.
“Tutatoa taarifa zaidi kadri itakavyofaa na kikao chetu kilichopangwa kufanyika kwa njia ya simu, Alhamisi tarehe 15 Juni saa tatu asubuhi muda wa Uingereza kitafanyika kama ilivyopangwa,” imesema taarifa ya Acacia.
Post A Comment: