Wiki kadhaa baada ya Dogo Janja aka Janjaro kuweka wazi kwenye vyombo vya habari kuwa muigizaji Irine Uwoya ndiye anayemkosesha usingizi na angependa siku moja awe barafu wa moyo wake, Uwoya amemfungukia.
Janjaro aliwahi kusema kuwa, “Irene Uwoya nampenda tangu nikiwa mtoto, nimeshabandika sana picha yake maghetoni. Nampendaga sana na ni mtu ambaye nammezeaga mate.”
Muigizaji huyo ambaye amekuwa akitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo za wasanii wa Bongo Flava akihusishwa na mfano wa uzuri na mvuto, amekejeli ombi la Janjaro ambaye amedai ni mdogo wake mwenye matatizo yake binafsi.
“Yaani kale jamani… ni mdogo wangu, naongeaga naye tunapiga story. Kananifurahisha lakini, hivyo tu,” Uwoya alisema
Hata hivyo, Uwoya aliweka wazi kuwa katika kumchagua mwandani yake, umri sio kigezo cha kumpima mwanaume anayetaka kuwa naye.
Post A Comment: