ads

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia imetoa taarifa kwa umma na kueleza kuwa kamati iliyofanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini  haijawapa ripoti ambayo Rais John Magufuli amekabidhiwa jana.


Katika taarifa hiyo, Acacia wamesema hawajui ni kwa kiasi gani ripoti hiyo itakuwa imeizungumzia kampuni hiyo lakini waliipa ushirikiano kamati hiyo wakati ikifanya uchunguzi.

Hata hivyo Acacia wamesisitiza kuwa huwa inatoa taarifa kamili ya kila kitu chenye thamani ya kifedha ambacho wanazalisha na huwa wanalipa kodi zote stahiki kwa kila madini yanayotakiwa kulipiwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: