
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Kumekuwa na kitendawili juu ya uwezo wa wanyama kuweza kutambua hisia za binadamu kwa kuwaangalia, huku ikielezwa kuwa ni mbwa pekee ndiye mnyama ambaye angeweza kutambua hisia kwa mtindo huo.
Lakini hivi karibuni, Wana sayansi wa Chuo Kikuu cha Sussex cha Uingereza wamefanya utafiti na kubaini kuwa farasi wana uwezo pia wa kubaini hisia za binadamu aliyekasirika au mwenye furaha kwa kumuangalia tu.
Wanasayansi hao walitumia picha za wanaume wenye tabasamu na wengine wenye hasira na kuwaonesha farasi 28 waliochaguliwa kufanyiwa majaribio na walitoa majibu sahihi.
Amy Smith ambaye alishiriki katika utafiti huo alieleza kuwa farasi walionesha hali ya uoga walipoona picha ya mwanaume aliyekasirika, na walitulia walipoona picha ya mwanaume aliye tabasamu.
Ilielezwa kuwa farasi walioneshwa picha ya mtu aliyekasirika waliiangalia kwa jicho la kushoto zaidi. Sayansi inaonesha kuwa akili za wanyama zimeumbwa katika hali ambayo hisia zinazotolewa na jicho la kushoto huangaziwa na eneo la kulia la ubongo ambalo hutumiwa kuangazia hisia mbaya.
Kadhalika, watafiti hao walieleza kuwa farasi waliooneshwa picha ya mtu aliyekasirika, mapigo yao ya moyo yalienda mbio zaidi ya pale walipooneshwa picha ya mwanaume aliyetabasamu.
Post A Comment: