ads

Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa, Augustino Mrema ameliomba Jeshi la Polisi nchini kuacha kuhangaika na watumiaji wa madawa ya kulevya (mateja) wasiojiweza na kuwapeleka magereza bali wasaidiwe kwa kupelekwa vituo vya kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya.


Mrema aliyazungumza hayo leo katika kipindi cha East Africa Breakfast cha EA radio na kusisitiza, jeshi la polisi linapaswa kuhakikisha wanaowapeleka magereza wawe mapapa wa dawa za kulevya ambao ni chanzo cha mateja nchini.

Alisema kuwa kuwakamata na kuwapeleka Magereza mateja ni sababu moja wapo ya msongamano wa wafungwa pamoja na wanachi kupenda kesi na visasi kwa kushindwa kumalizana mitaani.

"Wananchi wamekuwa sababu ya misongamano magerezani kwani kesi nyingine ni ndogo za kuweza kumalizana nyumbani lakini wanaamua kukomoana kwa kupelekana polisi hadi kufikia kufungana," Alisema Mrema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: