ads

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atawapumzisha baadhi ya wachezaji wake katika mechi ya siku ya Jumapili dhidi ya Arsenal.


Ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya klabu ya Uhispania Celta Vigo siku ya Alhamisi ulikuwa wa 10 tangu mwezi Aprili.

Huku kikosi hicho cha Mourinho kikiwa katika nafasi ya tano katika Msimamo wa ligi ya Uingereza, ligi ya kombe la Europa inaweza kuwapatia fursa ya kushiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao.

”Wachezaji ambao wameshiriki katika mechi nyingi hatawachezeshwa wikendi”, alisema Mourinho.

Mpira wa adhabu wa Marcus Rashford uliipatia United ushindi katika mchezo wakwanza  na nchini Uhispania huku mcezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa siku ya Alhamisi ijayo katika uwanja wa Old Trafford.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: