Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajia kufanya mazungumzo ya pamoja katika  mkutano wa kawaida wa  18 utakaofanyika leo (Jumamosi), Ikulu jijini Dar es salaam. 


Mkutano huo unatarajiwa kupokea  ripoti ya usuluhishi ya kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuhusu mgogoro wa Burundi.

 Mambo mengine yatakayozungumzwa katika mkutano huo ni pamoja na taarifa na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa katika mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo.

 Masuala hayo ni pamoja na namna ya kuwezesha uundaji wa magari katika   Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupunguza uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka nje ya Jumuiya, mapitio kuhusu sekta ya nguo na ngozi.

Masuala mengine ni pamoja na  kuzuia ama kuondoa uagizaji wa nguo na viatu vya mtumba kutoka nje.

Wakuu hao wa Nchi pia wanatarajia kujadili namna endelevu ya uchangiaji wa bajeti ya Jumuiya hiyo kwa nchi wananchama.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: