
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter wa klabu ya soka ya Everton, umethibitisha kuwa klabu hiyo kuwasili nchini mwezi Julai na itakuwa ni timu ya kwanza inayoshiriki Ligi kuu nchini Uingereza kucheza na timu za Afrika mashariki.
Ujio wa Everton ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi, Vilabu vinavyo tarajiwa kunufaika na ujio huo ni vile ambavyo vipo chini ya udhamini wa kampuni ya Michezo ya kubashiri ya SportPesa. Kwa hapa nchini mpaka sasa kampuni hii imeingia mkataba na klabu tatu ambazo ni Simba SC, Yanga SC pamoja na Singida United .
Kwa mujibu wa Kampuni ya SportPesa, wameandaa ligi ijulikanayo kama SportPesa Super Cup , inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 5 / 6 / 2017, kwa kushirikisha jumla ya timu 8 kutoka mataifa mawili, Tanzania na Kenya, na mshindi wa mashindano hayo atacheza na timu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.
Mshindi wa michuano hiyo mikubwa atapata kiasi cha Dola za kimarekani Elfu thelathini (USD 30,0000) na mshindi wa pili wa michuano hiyo anatarajia kupata kiasi cha Dola za kimarekani Elfu kumi (USD 10,000).
Kutokana na kuthibitisha kwa klabu ya Everton bilashaka mshindi wa mashindano hayo atacheza na klabu hiyo kongwe iliyoanzishwa mwaka 1978.
Post A Comment: