ads

Rais John Magufuli amevunja Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na kuagiza mali na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na mamlaka hiyo zihamishiwe halmashauri ya manispaa ya Dodoma.

Rais Magufuli pia amevunja bodi ya CDA hivyo  aliyekuwa mkurugenzi  mkuu wa bodi hiyo, Paskasi Muragili atapangiwa kazi nyingine na ameagiza wafanyakazi wote wa mamlaka hiyo wahamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na ofisi nyingine za Serikali kadri inavyofaa.

Rais Magufuli amevunja CDA kwa kutia saini hati ya amri ya Rais ya kuivunja mamlaka hiyo.

Amesema ameamua kuivunja mamlaka hiyo na kuhamishia majukumu yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kuondoa mkanganyiko wa utoaji huduma kwa wananchi uliokuwa ukisababishwa ma mgongano kati ya vyombo hivyo viwili.

Pia amesema ni kwa ajili ya kuendana na mahitaji ya sasa ambayo yamedhihirishwa kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa CDA.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: