ads

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB, Harmonize  ameweka wazi kiasi cha pesa anachoingiza kupitia mtandao wa Youtube kwa Mwezi .


Harmonize amesema watu wanashangaa kuona anatembelea magari ya kifahari ila hawajui tu kuwa muziki unampa Connections nyingi kwani mbali na show pia anaingiza mkwanja mrefu kupitia mtandao wa Youtube ambapo amefunguka kuwa anaingiza kiasi cha Dola za Kimarekani 3,500 kwa mwezi.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu Kupitia muziki umenikutanisha na watu wengi,Umenipa Dili napata riziki kwenye njia tofauti tofauti,sio tu kwenye show,licha ya kufanya show nauza nyimbo zangu kwenye Platform,Mimi akaunti yangu ya Youtube kila mwezi nalipwa Dola 3,500“Amesema Harmonize kwenye mahojiano yake na kipindi cha leo tena cha Clouds FM.

Harmonize kwa sasa ambae anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Niambie’ anatarajia kuanza Tour yake ya muziki wikiendi hii mkoani Mtwara.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: