ads

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeweka mikakati mitano ya kuboresha ukusanyaji kodi ya majengo, ikiwamo kutathmini majengo ili kupanga viwango rafiki vya kodi kwa walipakodi.


Mikakati mingine ni kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa ukusanyaji, kutoa elimu kwa jamii kuhusu ulipaji kodi, kushughulikia pingamizi za kodi kwa wakati na kuboresha orodha ya uthamini ili kuwa na takwimu sahihi.

Ofisa Msaidizi wa Huduma ya Mlipakodi ya TRA, Maya Magimba alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu umuhimu wa kodi.

Alisema kodi ni muhimu kwa Serikali kwa vile inatumika kuendesha shughuli za kijamii, ukiwamo ujenzi wa miundombinu ya barabara, zahanati na madarasa.

“Tutahakikisha nyaraka za usajili zinatunzwa na mlipakodi  kwa  kufuata taratibu ili kuepuka usumbufu,” alisema.

Alisema kodi ya majengo hulipwa kuanzia Januari mosi hadi Machi 31 kila mwaka bila adhabu, na baada ya Aprili mosi hulipwa na adhabu, kodi ya pango la ardhi hulipwa kuanzia Julai mosi hadi Desemba 31 kila mwaka.

Mkuu wa Kitengo  cha Habari na Mawasiliano Serikalini wa  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Mboza  Maige alisema  mwananchi au taasisi yenye nyaraka za umiliki wa ardhi ya Serikali anapaswa kulipa kodi hiyo.

Alisema iwapo eneo litakuwa na maendelezo ya jengo la kudumu na linatumika, mtu huyo atalazimika kulipa kodi mbili.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: