Timu ya KRC Genk anayocheza Mtanzania Mbwana Ally Samatta imeshindwa kutamba ugenini dhidi ya wenyeji CeltA Vigo baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-2 mchezo wa robo fainali wa Europa League.
Kwa matokeo hayo Genk wamejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwani wanahitaji ushindi wa goli moja tu ili waweze kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo.
Magoli ya KRC Genk yalifungwa na Jean Boetius dakika ya 10 na Thomas Buffel aliyeingia akitokea benchi dakika ya 68, kwa upande wa wenyeji magoli yao yalifungwa na Pione Sisto dakika ya 15, Iago Aspas dakika ya 17 na John Guidetti dakika ya 38, kipigo hicho kinailazimu Genk katika mchezo wa marudiano Luminus Arena April 20 itabidi wapate ushindi wa kuanzia goli 1-0 ili wafuzu nusu fainali.
Post A Comment: