ads

Msanii wa muziki wa hip hop, Chidi Benz amedai amejifunza vitu vingi kwa kipindi cha miezi mitatu alichokaa rehab mkoani Tanga na Iringa kwa ajili ya kusaidiwa kuacha matumizi ya dawa za kulevya.


Akiongea katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, Chid Benz amedai kukaa rehab kwa miezi mitatu bila tatizo ni mafanikio mapya katika maisha yake.

“Nimejifunza vitu na ninaendelea kujifunza vitu,” alisema Chidi. “Nimekaa muda mrefu zaidi maana sijawahi kukaa rehab miezi mitatu na ndio maana unaona nimetulia mpaka sasa hivi. Nina miezi miwili toka nimetoka niko poa niko freshi,”

Katika hatua nyingine rapa huyo amemtaka mwanaharakati wa kupambana na dawa za kulevya, Kalapina, kujifunza mbinu mpya ili aweze kuwasaidia vijana wa aina mbalimbali ambao wanakumbwa na tatizo hilo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: