KATIKA kutekeleza agizo la Rais John Magufuli, uongozi wa Jiji la
Arusha umeanza mchakato wa kujenga jengo la kufanyia shughuli za
biashara wafanyabiashara wadogo maarufu ‘Wamachinga.’
Eneo lililotengwa kwa mradi huo lipo katikati ya Jiji, kwenye kiwanja
Namba 69 chenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja, sehemu ambayo
ilirejeshwa serikalini na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ziara
yake mkoani Arusha hivi karibuni.
Kiwanja hicho kilichopo mkabala na soko la Kilombero, linadaiwa awali
liliuzwa kinyemela na madiwani wa halmashauri, kabla ya Waziri Mkuu
kuamuru lirudishwe na tayari eneo hilo limerudi serikalini.
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,
Athumani Kihamia alisema eneo hilo lina uwezo wa kuhifadhi
wafanyabiashara wadogo zaidi ya 2,000 pamoja na shughuli mradi
utakapokamilika. Jiji la Arusha lina wakazi takribani 500,000.
Mmoja wa machinga anayeuza viatu, Hussein Issa, amesema hilo ni jambo
jema, huku akushauri kusiwe na urasimu wakati wa ugawaji wa maeneo
yaliyotengwa kwa ajili yao.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: