
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel Tanzania imelipa zaidi ya Sh
milioni 687 baada ya kupewa siku saba na halmashauri hiyo iwe imelipa
fedha hizo ambazo zilikuwa za kodi ya pango inazodaiwa na manispaa hiyo.
Fedha hizo zililipwa Desemba 21 na mkataba huo wa zamani unaisha
Januari mwakani ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema
wanaandaa mpya wenye viwango vya malipo vya sasa.
Aidha halmashauri hiyo imeamua kuelekeza fedha hizo ambayo ni sh
687,931,040 katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 40 katika halmashauri
hiyo kwamba kama itaonekana inawezekana kujenga shule nyingine mpya ya
sekondari.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Hapi
alisema fedha hizo zimelipwa baada ofisi yake kubaini mchezo mchafu
uliokuwa umefanywa na watendaji wa halmashauri yake waliokuwepo huko
nyuma ambao walificha mkataba kati yake na Zantel.
Aidha aliipongeza Zantel kwa kutii maagizo waliyopewa na kulipa fedha
hizo na tayari wamepewa risiti kuonesha kupokea fedha hizo na kwamba
watu wote waliohusika katika jambo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.
Alisema baada ya malipo hayo, ameelekeza Manispaa kutumia fedha zote
hizo kujenga vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo.
“Takwimu zinaonesha mwaka huu watoto 19,000 walifaulu katika
Halmashauri ya Kinondoni waliochaguli kujiunga na Sekondari ni 12,889 na
hadi sasa wanafunzi 3,169 hawajapata nafasi katika shule zetu kwasababu
ya ufinyu wa madarasa,” alisema Hapi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: