Mtaalam wa upasuaji wa mfumo wa neva (neurosurgeon) Sergio Canavero
kutoka nchini Italia, anakusudia kufanya jaribio la kwanza la
kupandikiza kichwa cha binadamu kwenye mwili wa binadamu mwingine,
ifikapo mwakani.
Wataalam wengi wa upasuaji wanafikiria wazo hilo ni la
kiuwendawazimu, lakini sio kwa mtaalamu huyo, kwani anasema bado
anapanga kujaribu pandikizo la kwanza la kichwa kwa binaadamu. (Head
Transplant)
Dk. Canavero ambaye mpaka sasa ameshapata mtu wa kujitolea kufanya
zoezi hilo, kijana mwenye asili ya Urusi ambaye ni mtaalam wa software
Valery Spiridonov, ambaye ana tatizo la kupoteza nguvu kwa misuli yake
ya mwili.
Dk. Canavero amesema mafanikio yake yameonesha kuwa mpango wake wa
kupandikiza kichwa cha binadamu kwa mwili wa mtoaji (donor) bado upo, na
ataanza mpango huo mwishoni mwa mwaka 2017 na unaweza kuwa njia ya
kutibu waliopooza mwili.
“Ningesema tuna takwimu nyingi zinaendelea, ni muhimu kwa watu kuacha
kufikiria jambo hili sio rahisi, hii inawezekana kabisa na tunaendelea
kulifanyia kazi”, alisikika Dk, Canavero akimwambia mwanasayansi
mchanga.
Timu iliyo nyuma ya kazi hiyo ilipost video ikimuonesha nyani ambaye
alifanyiwa upandikizwaji huo, na kufanikiwa kutembea baada ya uti wa
mgongo kutenganishwa na kuunganishwa tena'
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: