ads

Baada ya lile drama kati ya nyota wa Bongo movie, Niva Supermariyo, na Nay wa Mitego kushika moto kutokana na wimbo wa 'Shika adabu yako' ya Nay na Niva kuamua kumjibu kupitia filamu ambayo aliipa jina la 'Maisha ya mtoto wa Manzese'.


Sasa mastaa hao wameamua 'kuvuana nguo' hadharani kwa kila mmoja kuamua kumponda mwenzake.

Wakizungumza na eNewz kwa wakati tofauti tofauti ili mastaa hao waweke bayana tofauti zao lakini waliamua kutoleana uvivu kwa kupigana madongo ya live bila kukwepeshana.

Alipoulizwa Niva kwanini aliamua kuingia kambi ili kuandaa filamu tu itakayo mponda Nay ? Niva alisema “Nay ni kama Babaji kwahiyo hawezi shindana na mimi haniwezi kama yeye alizoea kuwaonea wanyonge mimi sasa haniwezi, kimaisha kwanza hajanifikia na mtu mwenye akili huwezi kujianika sana vitu vyako vya ndani kama yeye anajiona staa, kwanini anakimbiwa na wanawake ?”.

eNewz haikuishia kufanya mahojiano na Niva, Ilitulazimu kumtafuta Rapper Nay wa Mitego kujua nini mtazamo wake kuhusu maneno ya Niva. Nay wa Mitego alifunguka maisha anayo ishi Niva pamoja na gari alilopewa na Muhindi.

“Kwa sehemu ambayo ninauhakika nayo kwa asilimia mia moja ni kwa Niva, Niva hana geto hana gari na alipewa na Muhindi, alipeleka movies namfahamu vizuri, Mimi natokea mtaani naimba sifanyi movie kwahiyo siishi maisha ya kuigiza,” Alisema Nay.

Aidha Niva ametoa sababu ya kutokuwepo sokoni kwa movie hiyo hadi sasa ni kutokana na kuzuiwa na uongozi wake baada ya kuona haina maana kutengeneza filamu kwa lengo la kujibishana na mtu na kumwambia kuwa anayeanza anaweza asionekane mgomvi ila anaye malizia akaonekana kuwa ndio mgomvi.

 Lakini amesema kuwa Nay wa mitego akiendelea ataiachia tuu huku Nay akimtaka Niva kuonyesha mahali anapoishi kama alichoimbwa ni uongo.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: