ads
LICHA ya kuzagaa kwa tetesi juu ya uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, mwanamitindo Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amesema kutokana na kuumizwa na mapenzi mara kwa mara, kwa sasa hajaona mwanaume wa kumuamini hivyo anaelekeza nguvu na akili zake kwenye kazi.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Jokate alisema ni ngumu kwa watu kuamini kuwa amekuwa akiumizwa na mapenzi mara kwa mara, kutokana na muonekano wa urembo alionao, lakini ukweli unabaki kuwa, anaumizwa na mapenzi na kwamba hana imani tena na wanaume.
“Kwa muonekano wangu wa juu, ni ngumu sana kuamini kuwa huwa naumizwa na mapenzi, hakika huwa naumia mno, kila ninayemuamini, anaishia kuniliza, sasa yatosha, simuamini mtu tena, sijamuona wa kumpa imani yangu kimapenzi, acha nielekeze nguvu na akili zangu kwenye kazi,” alisema Jokate.

Katikati ya wiki hii, Ali Kiba alinaswa Morogoro akiwa na mwanamke mwingine katika mazingira ambayo yaliashiria wana uhusiano wa karibu na kufanya watu waibue maswali.
GPL
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: