Tetesi za usajili ndani ya klabu
ya Yanga zinasema kwamba, mshambuliaji wake, Rais wa Liberia, Kpah
Sherman anakaribia kutua katika klabu mojawapo inayoshiriki ligi kuu
nchini Afrika Kusini.
Winga aliyekosa nafasi katika
kikosi cha kwanza cha Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho anatafutiwa timu
itakayomnunua baada ya BDF XI ya Botswana kutaja pesa dau dogo la
milion 10 za Kitanzania. Hata hivyo St.George ya Ethiopia wameonesha
kuvutiwa na Coutinho.
Yanga imepanga kumalizana na
kiungo mkabaji wa Gor Mahia , Khalid Auch pamoja na mshambuliaji Michael
Olunga ambaye Azam FC na Simba SC wanawania saini yake pia.
Beki kiraka, Mbuyu Twite yupo
mashakani kuendelea kukipiga Jangwani huku tatizo haswa imekuwa usumbufu
kutoka klabu yake ya zamani ya FC LUPOPO.



Post A Comment: