Watu watatu wamefariki wawili kati yao wanasadikiwa kuwa ni wafuasi wa Al Shabaab katika mapigano baina yao na jeshi la Polisi.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro amesema tukio hilo limetokea eneo la
mpakani mwa mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero na mkoa wa Tanga ambapo watu hao walikuwa wamejificha msituni.Amesema jeshi hilo linawashikilia watu sita kwa kuhusika na tukio hilo, na kwamba uchunguzi zaidi unafanyika ikiwa ni pamoja na msako mkali katika eneo hilo.
Taarifa kutoka katika hospitali ya mission ya Turian mkoani Morogoro zinasema kuwa maiti tatu zimehifadhiwa hapo ambapo kati ya hizo,maiti mbili zinaonekana kuwa ni za watu wasio raia wa Tanzania huku moja ikiwa ni ya mtu ambaye alijeruhiwa vibaya na badaye kufariki akiwa hospitalini hapo.
Post A Comment: