ads

Rais John Magufuli, amesema watapitia upya na kuchambua uongozi wa Benki ya Wanawake nchini (TWB), ili benki hiyo iweze kufanya kazi kiushindani.


Rais Magufuli amesema hayo jana Desemba 8, mjini Dodoma wakati akizindua mkutano wa tisa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kuongeza kuwa benki hiyo imekuwa ikimkandamiza mwanamke hasa katika mikopo kwa kulipia riba kubwa na wakati huo huo wanufaika wengi wa mikopo hiyo ni wanaume.

“Tutapitia upya na kuichambua Benki ya Wanawake, hatuwezi kuwa na benki inayowaumiza wanawake tutaiangalia ili iende vizuri kiushindani, hatuwezi kuwa na benki ambayo inafanya ufisadi tu isiwe chombo cha kuleta hasara kwa fedha ambazo zingeweza kwenda kwenye kilimo lakini wanaokopa pale ni wanaume,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli ameutaka uongozi mpya atakaouchagua kumsaidia kufanya mabadiliko katika benki hiyo ili ifanye kazi kwa ufanisi na ushindani.

“Kumekuwa na kawaida kuwa benki hii kila anapokuwa mwanamke haifanyi vizuri badala yake imekuwa ya kuwanyonya wanawake, nimesema haya na ni matumaini yangu mmenielewa,” amesema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: