ads

Ofisi kuu ya Rais wa Nigeria imethibitisha kuwa wanafunzi 82 wa shule ya wasichana wa Chibok, waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram mnamo mwaka wa 2014,
wameachiwa huru.

Maafisa wanasema kuwa waliachiwa huru, kufuatia majadiliano ya muda mrefu na ubadilishanaji washukiwa wa Boko Haram, waliokuwa wamezuiliwa na wakuu wa nchi hiyo.

Wasichana hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na Cameroon, hayo ni kwa mjibu wa mwaandishi habari wa BBC Stephanie Hegarty kutoka Lagos.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: