ads

Matajiri wa Ufaransa, Klabu ya soka ya Paris Saint-Germain yaweka mezani dau la Euro Milioni 70  kwa klabu ya  Borussia Dortmund ili wapate saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.


Taarifa kutoka ndani ya PSG zinakanusha habari hizo zilizoandikwa na gazeti la Bild la nchini Ujerumani kwamba mzaliwa huyo wa Ufaransa, ambaye amefunga jumla ya mabao 35 msimu huu, tayari amekutana na Mkurugenzi wa Soka wa PSG, Patrick Kluivert mjini Paris.

Aubameyang, mwenye umri wa miaka 27, kama dili hilo litafanikiwa,  atakuwa anaingiza kitita cha Euro Milioni 14 kwa msimu akitua PSG, pato ambalo ni mara mbili ya mshahara wake wa sasa.

Taarifa zinasema kuwa Dortmund inajipanga kupokea ofa ya PSG msimu utakapomalizika baada ya fainali ya Kombe la Ujerumani Mei 27 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Kwa upande wa mchezaji huyo mara kwa mara amesikika akisema kuwa anataka kujiunga na kikosi cha Mfaransa, Zinedine Yazid Zidane,”Zizou” , kocha wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: