ads

Kufuatia ajali iliyotokea jana Mkoani Arusha na kuua watu zaidi ya 30, Chama Cha Mapinduzi kimetuma salamu zake za rambirambi na pole na kuongeza kuwa msiba huo wameupokea kwa masikitiko makubwa sana


Salamu hizo zimetolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndg, Humphrey Polepole na kusema kuwa Chama Chama Mapinduzi kimepokea taarifa za ajali na vifo hiovyo kwa masikitiko makubwa kwa kuwa wanafunzi hao walikuwa katika safari ya kujiimarisha kiitaluma ili kutimiza malengo yao na

"Taifa limepoteza raia wema na nguvu kazi ya sasa na baadae. Chama kinatambua kuwa safari hiyo waliyokuwemo watoto hawa ilikuwa sehemu ya kuwaimarisha kitaaluma ili kutimiza ndoto zao maishani"-  Humphrey Polepole

Aidha Katibu Mkuu wa Chama hicho Comrade Abrahman Kinana ameungana na Watanzania wote kupitia msiba huo na kusema kwamba

"Licha ya kwamba wapendwa wetu wametangulia mbele za haki , wataendelea kubaki katika kumbukumbu zetu daima na tunamuomba Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina. Tunawaombea Kupona haraka majeruhi wote waliotokana na ajali hiyo"- Abrahman Kinana.

Ajali hiyo imetokea jana Mkoani Arusha, Wilayani Karatu baada ya basi walilokuwa wamepanda wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent jijini Arusha walipokuwa wakienda kufanya mtihani wa ujirani mwema katika shule ya Tumaini kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo eneo la Rhotia Marera, ambapo limeua zaidi ya watu 30 wakiwepo wanafunzi, waalimu na dereva wa basi hilo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: