ads

Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe ametoa pole kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali iliyotokea jana Jijini Arusha na kusababisha vifo zaidi ya 30.


Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Nzega amewatia moyo wanafamilia wote na Taifa kwa ujumla kufuatia msiba huu na kuwataka watanzania wote kuwa tayari kwa safari hii.

"Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nzega niwape pole familia za watoto hawa waulim na madereva ambao mwenyezi Mungu amewaita mbele ya haki" - Hussein Bashe.

"Kila nafsi itaonja mauti na mwenyezi Mungu amewaita hawa binadaam wenzetu katika umri mdogo wakati wazazi wao, familia zao na Taifa likiwa na matarajio makubwa na matumaini makubwa, ila Allah hutupima imani zetu kwa majaribu makubwa kama haya, tumshukuru kwa kila jambo na sisi tujiandae kwa safari hii ya asili na kimaumbile" - aliongeza Bashe.

"Poleni wanafamilia, poleni walimu, poleni watanzania wote"- Hussein Bashe.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: