
Manchester United imekuwa
miongoni mwa klabu ambazo zimetambulisha jei zao zitakazotumiwa kwa
ajili ya msimu ujao. Klabu hiyo imevunja rekodi kwa kuwa ni klabu
inayopiga pesa nyingi duniani kutoka kwa watengezaji wa jezi ambapo jezi
zao zitakuwa zikitengenezwa na kampuni ya Adidas baada ya kusaini dili
la pauni milioni 750.
Kabla ya Adidas Nike ndio
walikuwa watengenezaji wa jezi za mashetani wekundu na wamedumu kwa muda
wa miaka 13 kabla ya Adidas kuchukua dili hilo baada ya mkataba wa Nike
na Man U kumalizika.
Wakongwe hao (Adidas) wa
kutengeneza vifaa vya michezo wanaamini wnaweza kutengeneza kiasi cha
pauni bilioni 1.5 kutokana na mauzo ya jezi za Man U kwa muda wa miaka
10 ijayo.
Dili hilo kati ya Manchester
United na Adidas linayapiku madili mengine ya klabu ambazo
zinatengenezewa jezi na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na klabu Bayern
Munich (pauni milioni 645) na Chelsea (pauni milioni 300).
Jezi hizo mpya zitakuwa na
muonekano kama ule wa zamani enzi za Ryan Giggs zikiwa na shingo ya V
yenye rangi nyeupe na michirizi mitatu kwenye mikono yake.
Post A Comment: