
England imepangwa pamoja na Ubelgiji na Tunisia na Panama huku Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wakipewa timu ngumu.
Katika upangaji wa ratiba hiyo England imepangwa Kundi G watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Ubelgiji katika kuwania nafasi ya kuongoza kundi hilo.
Kikosi hicho cha Gareth Southgate kitafunga kampeni yake ya kusaka ubingwa wa kwanza wa dunia tangu 1966 kwa kucheza na wawakilishi wa Afrika, Tunisia Juni 18 kwenye Uwanja wa Volgograd.
England itacheza mechi ya pili dhidi ya Panama, kwenye Uwanja wa Nizhny Novgorod hapo Juni 24 kabla ya kumaliza na Ubelgiji kwenye Uwanaj wa Kaliningrad hapo Juni 28.
Ronaldo na Ureno wamepangwa Kundi B pamoja na mabingwa wa Dunia 2010, Hispania, Iran na wawakilishi wa Afrika, Morocco.
Wakati Messi ataiongoza Argentina katika Kundi D wakiwa na Croatia, Iceland na miamba ya Afrika, Nigeria.
Makundi Kombe la Dunia 2018
Kundi A: Russia, Uruguay, Misri, Saudi Arabia
Kundi B: Ureno, Hispania, Iran, Morocco
Kundi C: Ufaransa, Peru, Denmark, Australia
Kundi D: Argentina, Croatia, Iceland, Nigeria
Kundi E: Brazil, Uswisi, Costa Rica, Serbia
Kundi F: Ujerumani, Mexico, Sweden
Kundi G: Ubelgiji, England, Tunisia, Panama
Kundu H: Poland, Colombia, Senegal, Japan
Post A Comment: