
Kwa mara ya kwanza Real Madrid itacheza na Barcelona Jumamosi mchana Desemba 23 kwa mujibu wa ratiba ya LaLiga iliyotolewa kwa mechi za kabla Krismass.
Hii ni mara ya kwanza kwa miamba hiyo kukutana katika siku ya mwisho kabla ya kuanza kwa mapumziko ya sikukuu.
Baada ya Clasico Krismassi, michezo mingine itashudia Valencia ikiwakaribisha Villarreal na Deportivo La Coruna itakuwa nyumbani kuwakaribisha Celta Vigo kwenye Uwanja wa Riazor.
Mechi za mzunguko wa 17, zimetanywa katika siku mbalimbali huku Leganes ikicheza na Levante wataanza Jumanne, Desemba 19.
Mechi nyingine kubwa itashudia Real Sociedad ikivaa Sevilla, Desemba 20, timu za mkiani Malaga na Alaves zitakutana Ijumaa usiku Desemba 22.
Post A Comment: