
AFYA ya faru mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani anayehifadhiwa katika Bonde la Ngorongoro, maarufu kwa jina la Fausta, imeimarika baada ya kuugua kwa muda mrefu katika eneo maalumu alikohifadhiwa.
Faru Fausta amekuwa kivutio kikubwa kutokana na umri wake.
Kwa sasa faru huyo ametengwa kwa ajili ya kutibiwa majeraha makubwa aliyokuwa nayo kutokana na changamoto za porini.
Kwa mujibu wa daktari anayemuangalia faru huyo, Dk. Francis Makali, Fausta ana umri wa miaka 52.
“Fausta alikuwa na majeraha makubwa ambayo yalihatarisha maisha yake," alisema Dk. Makali, lakini "hivi sasa afya yake imeimarika na anaendelea vizuri.”
Alisema licha ya afya ya faru huyo kuimarika, hakuna mpango wa kumuachia arudi nyikani kutokana na umri wake kuwa mkubwa pamoja na uoni hafifu wa jicho moja.
Hivi karibuni faru fausta alizua gumzo bungeni,baada ya taarifa kusema kuwa matibabu yake na malisho yake kwa siku ni zaidi ya milioni 50
Post A Comment: